Church News, Covid - 19

MAELEKEZO YA JINSI YA KUENDELEA KUKABILIANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA (COVID-19)

Pokeeni salama za pekee kutoka makao makuu ya TAG – Dar es salaam. Tunamshukuru Mungu ambaye ameendelea kututunza na kutulinda hasa katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya Corona (COVID – 19) hapa nchini na duniani kwa ujumla. Kamati kuu ya Utendaji ya Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa niaba ya Halmashauri kuu ya TAG inapenda kuwashukuru wote kwa kuendelea kuzingatia maelekezo ambayo tumeendelea kuyatoa kwa nyakati tofauti katika kuendelea kukabiliana na janga hili Sambamba na maelekezo tuliyoyatoa hapo awali, tunatoa maelekezo ya ziada kama ifuatavyo:-

  1. Ibada za Maombi
    1. Tunaamini kuwa maombi ndio jiu pekee la hili janga. Hivyo basi Kamati Kuu ya Utendaji inaelekeza kuwa maombi yasikome makanisani na kwa washirika binafsi. (1 Thes 5:17 “Ombeni bola kukoma”).
    2. Kama tuivyoelekeza kwenye barua zetu za awali, siku ya Ijumaa iendelee kuwa siku ya kufunga na kuomba kwa dhidi ya janga hili.
    3. Wiki ya tarehe 25 – 31 Mei 2020 (yaani ya Pentekoste) itakuwa ni wiki ya Maombi Maalum ya mapatano ya kufunga na kuomba kwa kanisa zima la TAG kwa ajili ya kuomba dhidi ya janga hili. Tafadhari zingatia kuwa maombi haya sio ya mnyororo au kupokezana bali ni ya mfululizo kwa kanisa zima.
    4. Bado inaaminika kuwa hakuna chanjo wala tiba ya ugonjwa huu wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona. Hivyo kama kanisa tunaendelea kumuomba Mungu ili chanjo na tiba ya ugonjwa huu ipatikane.
  2. Tahadhari na Kujikinga
    1. Tunahimiza kuwa kila mmoja wetu (Kiongozi, Mchungaji na Mshirika) ajilinde mwenyewe na kuwa mlinzi wa mwenzake. Pamoja na kuwa hatma ya afya ya kila mmoja wetu iko mikononi mwa Mungu, lakini pia ushindi upo kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua madhubuti kujikinga na maambukizi ya COVID-19 (Efes 5:17, “Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana”). Hivyo tunashauri kila mmoja wetu kuzingatia yafuatayo
      1. Kuepuka sehemu za mikusanyiko mikubwa.
      2. Kuepuka safari au mizunguko ya hapa na pale isiyo kuwa ya lazima.
      3. Kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara.
      4. Kutumia vitakasa mikono (sanitizer) mara kwa mara.
      5. Kuzingatia uvaaji wa barakoa kama inavyoelekezwa na wataalamu wa afya.
      6. Kujitahidi kupata mlo kamili na kula vyakula vyenye vitamini C kwa wingi (matunda na mboga mboga) ili kuimarisha kinga ya mwili
      7. Kujitahidi kufanya mazoezi ya mwili ili kuimarisha afya.
      8. Kuzingatia kikamilifu maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya, Serikali na Shirika la Afya Duniani
      9. Kutoa taarifa kituo cha afya au mamlaka husika pale utakapojihisi dalili au utapomuona mtu mwenye dalili za ugonjwa huu kama zilivyoainishwa na Wizara ya Afya.
    2. Tunahimiza ibada za ndoa zihudhuriwe na watu wachache iwezekanavyo na zisiwe na shamrashamra zinaweza changia maambukizi.
    3. Tunahimiza ibada za mazishi ziendeshwe kwa umakini wa hali ya juu na kuhudhuriwa na watu wachache iwezekanavyo ili kuepuka kusambaa kwa maambukizi.
  3. Kamati za Ushauri za Afya
    1. Kamati kuu ya Utendaji inaelekeza kuwa kila Jimbo, Sehemu na Kanisa la mahali pamoja liunde “Kamati ya Ushauri ya Afya”
    2. Tunapendekeza wataalamu wa afya waliopo makanisani mwetu wawe sehemu muhimu ya kamati hizi.
    3. Kamati hizi zitakuwa na jukumu la kufuatilia kwa karibu mwenendo wa COVID-19 pamoja na hatua ya kukabiliana na janga hili katika ngazi husika na kutoa ushauri au maelekezo pale inapobidi.
    4. Kamati hizi pia zitatoa elimu za mara kwa mara katika ngazi husika juu ya jinsi ya kuendelea kujikinga na janga hili la Corona kulingana na miongozo ya Wizara ya Afya.
  4. Wajibu wa Kanisa kwa Jamii
    1. Kama kanisa na kwa mujibu wa mpango mkakati wa miaka 13 ya moto wa uamsho, tunalo jukumu la kuonesha upendo wa Kristo kwa jamii inayotuzunguka.
    2. Kamati kuu ya Utendaji inaelekeza Majimbo yote na idara za kanisa Kitaifa kutumia mwezi Mei na Juni kutoa misaada mbalimbali kwa taasisi za Serikali na Jamii zinazoshughulika moja kwa moja na waathirika wa COVID-19. Misaada hii inaweza kuwa barakoa, gloves, vitakasa mikono, mavazi ya kujikinga na vifaa vingine vya afya.
    3. Kwa sababu hili suala linaigusa jamii, tunashauri zoezi la makabidhano ya vifaa lifanyike kwa uwazi
    4. Majimbo na idara zitoe taarifa ya kimaandishi ya utekelezaji wa mambo haya kabla ya tarehe 20 Juni 2020 kwa Katibu Mkuu wa TAG.

Write A Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ready to get started ?

Speak to Uwezo Financial +255 786 670 921

×